Sala
Kwa Ajili ya Jumuiya ya Mwenye Heri Gérard
Bwana Yesu Kristu,
Kwa neema yako umeniita nikutumikie
katika Shirika la Mwenyeheri Gerhard.
Nakushukuru kwa kunijalia neema hiyo.
Kwa maombezi ya Mama yetu Maria,
Mtakatifu Yohane Mbaptizaji, Mwenyeheri Gerhard na watakatifu wote, kwa
unyenyekevu naomba ili roho ya shirika letu ipenye maisha na matendo yangu ili
niweze kujitoa kwa utumishi katika familia yangu, kati ya rafiki na yeyote
mwenye kuhitaji msaada wangu.
Nikitumainia msaada wako, nataka daima
niilinde imani na niwe na mapendo kwa jirani, hasa maskini, wenye huzuni,
wapweke, vilema na wagonjwa.
Nipe nguvu ninayohitaji kwa
kuishi kadiri ya matakwa hayo kama
Mkristu wa kweli anayejitolea nikitimiza maneneo ya Injili yako
Kwa ajili ya utukufu ya
Mungu, amani duniani na ustawi wa shirika letu.
Amina
We thank Fr. Pius Mühlbacher O.S.B. and Br. Polykarp O.S.B. for this translation into
Kisuaheli.
Bwana Yesu Kristo,
Kwa njia ya neema zako umeniita Mimi
kukutumikia kama mwanajumuiya ya Mwenye Heri Gérard.
Ninakushukuru kwa kuniteua kwa wajibu
huu.
Kwa maombezi ya Mama yetu, Mtakatifu
Yohane Mbatizaji, Mwenye Heri Gérard
na watakatifu wote, ninakuomba kwa unyenyekevu ili Maisha ya kiroho ya
Jumuiya yetu yapenye Maisha na matendo yangu katika kujitoa kwa ajili ya
utumishi wa familia yangu, marafiki zangu na yeyote anayehitaji msaada wangu.
Nikitegemea msaada wako, ninataka kila
mara kulinda imani na kuwa na moyo ulio wazi kwa jirani hasa masikini, wenye
huzuni, wapweke, wasiojiweza na wagonjwa.
Unijalie nguvu inayohitajika kuishi
kama Mkristo muadilifu kulingana na roho ya Enjili na kulingana na
uamuzi wangu.
Kwa ajili ya sifa na Utukufu wa Mungu,
kwa ajili ya amani duniani na kwa faida ya jamii yetu.
Amina.
We thank Br. Markus Forster O.S.B. for this translation into
Kisuaheli.
Back to the homepage of the Brotherhood of Blessed
Gérard
This page was last updated on
Dienstag, 30 Juni 2020 12:13:18